Ugawaji wa Viwanja na Mashamba
Kugawa mashamba makubwa na maeneo kuwa viwanja vidogo vilivyopimwa vyenye ramani na njia bora za barabara.
Kuhusu Huduma Hii
Iwe unataka kugawa shamba la urithi wa familia, kugawa eneo la biashara Kisongo, au kutekeleza mradi wa viwanja vya makazi, RELAND inatoa huduma kamilifu ya ugawaji wa ardhi. Tunasimamia uchoraji wa ramani, ufunguaji wa barabara, uwekaji wa beacons na kutoa hati miliki kwa kila kiwanja.
Mambo Muhimu Yanayotekelezwa (Deliverables):
Mchakato wa Kazi Hatua kwa Hatua
Kupima Mipaka ya Nje ya Shamba
Tunapima na kuhakiki mipaka ya shamba mama kwa GPS kuhakikisha ukubwa halisi.
Uchoraji wa Mchoro wa Ugawaji
Tunaandaa mchoro wa viwanja unaozingatia barabara, miundombinu na matumizi bora ya ardhi.
Idhini ya Idara ya Mipango Mji
Mchoro unawasilishwa na kuidhinishwa na Idara ya Mipango Mji na Halmashauri husika.
Uwekaji wa Vigingi & Hati za Kila Kiwanja
Tunaweka beacons kwa kila kiwanja na kuandaa Deed Plans kwa ajili ya hati miliki binafsi.
Maswali ya Kawaida Kuhusu Ugawaji wa Viwanja na Mashamba
Ukubwa wa chini wa kiwanja kinachoruhusiwa kisheria Arusha ni upi? +
Kulingana na kanuni za mipango miji, viwanja vya makazi ya msongamano mkubwa huanzia mita za mraba 300–400, na msongamano wa kati/chini huanzia SQM 600 hadi 1500+.
Wasilisha Mahitaji Yako
Wataalamu wetu waliosajiliwa watawasiliana nawe.