Ushauri wa Kitaalamu wa Ardhi & Uwekezaji
Ushauri makini wa ununuzi, ukaguzi wa nyaraka Wizarani, na mikakati salama ya uwekezaji wa ardhi.
Kuhusu Huduma Hii
Kununua au kuwekeza kwenye ardhi kunahitaji umakini na utaalamu wa kisheria. RELAND inatoa ushauri wa kitaalamu kwa wananchi, watanzania wanaoishi nje (Diaspora), na wawekezaji ili kuepuka utapeli, kuuziwa eneo lenye mgogoro au lililotengwa kwa matumizi ya umma.
Mambo Muhimu Yanayotekelezwa (Deliverables):
Mchakato wa Kazi Hatua kwa Hatua
Kupokea Nyaraka za Eneo
Mteja anawasilisha nyaraka au maelezo ya eneo analotaka kununua au kuliendeleza.
Ukaguzi wa Kina Wizarani
Tunafanya ukaguzi rasmi katika masjala ya Wizara ya Ardhi, TARURA, na Halmashauri.
Ukaguzi wa Eneo Shambani
Timu yetu inatembelea eneo kukagua mipaka, hali ya udongo, barabara na majirani.
Ripoti ya Ushauri wa Kitaalamu
Unapokea ripoti kamili ya maandishi inayokupa mwongozo salama wa kuendelea na malipo au kusitisha.
Maswali ya Kawaida Kuhusu Ushauri wa Kitaalamu wa Ardhi & Uwekezaji
Nipo nje ya nchi (Diaspora). RELAND inanisaidiaje kununua kiwanja salama? +
Tunakufanyia ukaguzi wa kina wa kisheria, video za eneo live, kupima mipaka na kusimamia uhamisho wa hati bila kutegemea madalali au kuingizwa kwenye mikataba hewa.
Wasilisha Mahitaji Yako
Wataalamu wetu waliosajiliwa watawasiliana nawe.