Upimaji wa Ardhi (Cadastral & Topographical)
Mwanzo / Huduma Zetu / Upimaji wa Ardhi (Cadastral & Topographical)
Upimaji wa Kina & Beacons

Upimaji wa Ardhi (Cadastral & Topographical)

Upimaji wa kisasa wa kijiografia, uwekaji wa beacons na kuandaa ramani rasmi za upimaji (Deed Plan).

Maelezo ya Kitaalamu

Kuhusu Huduma Hii

RELAND inatoa huduma za kitaalamu za upimaji wa ardhi (Cadastral & Topographical Surveying) jijini Arusha na kanda ya kaskazini. Kwa kutumia vifaa vya kisasa vya RTK GNSS na Total Station, wapimaji wetu waliosajiliwa wanapima mipaka kwa usahihi wa kiwango cha juu na kuandaa ramani zilizoidhinishwa na Wizara ya Ardhi.

Mambo Muhimu Yanayotekelezwa (Deliverables):

Ukaguzi, uhakiki na uwekaji wa beacons mpya za zege
Upimaji rasmi kwa ajili ya kuandaa Hati Miliki
Upimaji wa mwinuko na mandhari ya ardhi (Topographical Surveys)
Uandaaji wa ramani zilizoidhinishwa (Approved Deed Plans)
Upimaji wa miundombinu ya barabara, ujenzi na mifereji
Ramani za kisasa za kijiografia (GIS Maps)
Hatua za Utekelezaji

Mchakato wa Kazi Hatua kwa Hatua

01

Ushauri & Ukaguzi wa Kumbukumbu

Tunaanza kwa kukagua nyaraka zako na kufanya ukaguzi kwenye kumbukumbu rasmi za ramani Wizara ya Ardhi.

02

Upimaji wa Shamba kwa RTK GPS

Wataalamu wetu wanafika eneo la mradi na kupima mipaka yote kwa kutumia vifaa vya kiwango cha juu cha GPS na Total Station.

03

Uwekaji wa Beacons & Ushuhuda

Tunaweka vigingi na beacons rasmi za zege mbele ya wajumbe wa serikali ya mtaa na majirani wa eneo.

04

Uidhinishaji wa Ramani Wizarani

Tunaandaa na kuwasilisha ramani rasmi za upimaji (Deed Plans) kwa ajili ya kusajiliwa na Mkurugenzi wa Upimaji wa Ardhi.

Maswali ya Kawaida Kuhusu Upimaji wa Ardhi (Cadastral & Topographical)

Kwanini ninahitaji kupima ardhi kabla ya kujenga au kununua? +

Upimaji unakuhakikishia kuwa unajenga ndani ya mipaka yako halali na kukulinda dhidi ya migogoro ya kuingiliana na majirani au kununua eneo hewa.

Upimaji na uwekaji wa beacons unachukua muda gani Arusha? +

Upimaji shambani unachukua siku 1 hadi 3, na ukamilishaji wa mahesabu ya ramani unachukua wiki 1 hadi 2.

Direct Consultation

Wasilisha Mahitaji Yako

Wataalamu wetu waliosajiliwa watawasiliana nawe.